Mwaka
2021 ulimwengu utashuhudia mmarekani aliyefanikiwa zaidi kutekeleza
matukio ya ujambazi akitoka gerezani baada ya kutumikia kifungo cha
miaka 17 baada ya kufanikiwa kuishawishi serikali na mahakama kupunguza
kifungo chake kutoka miaka mia moja kumi na tano (115) mpaka miaka hiyo
17.
Atakapotoka
na kurudi uraiani atakuwa na miaka 69, jina lake anaitwa Carl Gugasian
au maarufu kama ‘The Friday Night bank robber’! Muhalifu aliyeiumiza
kichwa FBI kwa miaka 30 akitekeleza matukio 50 ya kuvamia na kuiba benki
pasipo kukamatwa kitendo kilichopelekea FBI na waendesha mashitaka wa
marekani ‘kumsifu’ kuwa ndiye muhalifu mwenye akili na aliyefanikiwa
zaidi katika historia ya marekani (the most prolific bank robber)
Kumekuwa
na kelele nyingi kutoka kwa ‘mashabiki’ wakiitaka Hollywood watengeneze
muvi kuhusu maisha ya ‘the friday night bank robber’!
Jambo
lililowashangaza wengi na ulimwengu wote ni jinsi gani binadamu mmoja
aliweza kutekeleza matukio 50 ndani ya miaka 30 akiwa peke yake na FBI
washindwe kujua identity yake wala kuwa na hata mbinu ya kuweza kumzuia
au kumkamata.
Mbinu,
weledi na nidhamu aliyokuwa nayo na kutumia kutekeleza matukio yake
yalikuwa ni siri na kitendawili mpaka pale alipokamatwa na kuamua
kuwasimulia FBI ili kujaribu kuwashawishi kumpunguzia adhabu ya
kifungo.. Na hii ni historia yake ‘kwa kifupi’ tu
ALIWEKA DHAMIRA AWE “MUHALIFU MWELEDI”Akiwa
na miaka 15 Carl alitekeleza tukio lake la kwanza la ujambazi ambapo
alijaribu kuiba fedha katika candy store bila mafanikio na alipigwa
risasi tumboni na kukamatwa. Baada ya kukamatwa alipelekwa katika jela
ya watoto ya Camp Hill kwa miezi 18.
Baada
ya kutoka jela Carl alidhamiria sasa kuwa ni lazima awe muhalifu mwenye
weledi wa hali ya juu kiasi kwamba atafanikiwa katika kila tukio na
hatoweza kukamatwa na akadhamiria kama anataka kufanikiwa aibe fedha
nyingi kwa wakati mmoja basi sehemu sahihi ya kuiba ni bank na kama
anataka kweli awe muhalifu mweledi anatakiwa ajue namna sehemu hizo
(majengo na mifumo) zinavyofanya kazi, afahamu namna ya kutumia silaha,
ajue namna ya kujihami (self defense) na namna atakavyo toroka na
fedha..
Baada
ya kuweka dhamira hiyo Carl akachukua hatua ya kwanza na alichofanya
ilikuwa ni kujiunga na Chuo kikuu cha Villanova ambapo alisomea Uhandisi
wa umeme. Akiwa chuoni alitumia mwanya huo kujiunga na programu maalum
ya jeshi la marekani kwa ajili ya kurecruit vijana walioko chuoni! Baada
ya kumaliza Chuo akaenda kutumikia jeshi kwa muda mfupi kituo cha Fort
Bragg na akiwa huko akapata mafunzo maalumu ya kijeshi (Special Forces
and tactical weapons training)
Baada
ya kupata mafunzo ya kijeshi Carl akarudi Chuo kusoma masters degree ya
System Analysis na alipomaliza masters degree akafanya mafunzo ya awali
kwa ajili ya shahada ya uzamivu katika Statistics.
Pia
mtaani alipokuwa anaishi alijiunga na kituo cha kufundisha mafunzo ya
kujihami (karate and judo) ambapo alifanikiwa kupata mkanda mweusi
(third degree black belt)
Baada
ya kufanikiwa kufanya maandalizi yote hayo na kupata kila aina ya
mafunzo na uzoefu aliyohitaji ili kuwa ‘muhalifu wa daraja la kwanza’
sasa ulikuwa ni wakati kwake kupita kila benki kukomba hela na
kuudhihirishia ulimwengu kuwa hakujapata kuwepo na itachukua miaka mingi
kutokea muhalifu professional kama yeye Carl ‘the Friday night bank
robber’..
MAANDALIZI KABLA YA TUKIO
Moja kati ya vitu vilivyomsaidia Carl kufanya matukio ya uhalifu kwa mafanikio ni uwezo wake wa kuweka mkakati wa utekelezaji jinsi gani atakavyofanikisha azma yake! Ni dhahiri kuwa mafunzo ya kijeshi aliyoyapata yalimsaidia sana kuwa mwanamkakati mzuri wa kiufundi wa matukio! Carl alikuwa anatumia had I miezi kadhaa katika kupanga utekelezaji wa tukio moja tu..
Moja kati ya vitu vilivyomsaidia Carl kufanya matukio ya uhalifu kwa mafanikio ni uwezo wake wa kuweka mkakati wa utekelezaji jinsi gani atakavyofanikisha azma yake! Ni dhahiri kuwa mafunzo ya kijeshi aliyoyapata yalimsaidia sana kuwa mwanamkakati mzuri wa kiufundi wa matukio! Carl alikuwa anatumia had I miezi kadhaa katika kupanga utekelezaji wa tukio moja tu..
Kwanza
kabisa Carl ali scout bank zilizopo katika miji midogo. Baada ya kupata
orodha ya benki katika miji kadhaa midogo then Carl aliangalia kati ya
bank hizo ni bank gani haziko katikati ya mji (kwa maana kwamba ziko
pembezoni/nje ya mji). Kisha Carl aliichagua bank moja wapo kati ya hizo
na bank ambayo inakuwa haiko karibu sana na makazi ya watu au iko
karibu na msitu basi bank hiyo anaipa kioaumbele katika orodha yake..
Baada
ya kuamua ni bank gani atafanya tukio, Carl alianza tafiti juu ya tukio
lenyewe atakavyolitekeleza… Kwanza kabisa Carl alianza kwa kusoma
mandhari yanayozunguka bank na interest yake kubwa inaelezwa kuwa
alitafiti zaidi msitu ambao unakuwa karibia na bank.. Inaelezwa kuwa
Carl angeutembelea msitu huo na kuukagua nukta baada ya nukta,
haijalishi ni muda gani angetumia mpaka kumaliza kuukagua!
Inaelezwa
kuwa lengo lake lilikuwa ni kujua ni maeneo gani ya msitu ambapo watu
huwa wanamazoea ya kupita au kutembelea, ni eneo gani la msitu
limejificha zaidi, ni upande gani wa msitu unakuwa rahisi kuifikia
barabara, ni eneo gani la msitu lina umajimaji na eneo gani ni kavu na
kadhalika na kadhalika.. Inaelezwa kuwa Carl angeutafiti huo msitu na
kuufahamu kuliko hata wenyeji wa eneo hilo husika.. Angeufahamu msitu
nukta kwa nukta!
Baada
ya kuufanyia tafiti msitu, inaelezwa kuwa Carl alikuwa anageukia
kuitafiti bank yenyewe na wafanya kazi wake.. Kuhusu bank, angetafiti je
hiyo bank inafungwa na kufunguliwa saa ngapi, ni siku zipi huwa
wanachelewa kufunga, ni siku gani wanakuwa na kiasi kikubwa cha fedha
n.k! Kisha akimaliza hapo anageukia kuwatafiti wafanyakaxi wa bank
husika.. Hapa alitafiti kuhusu ‘shifti’ zao za kazini, nanj ni teller,
nani ni manager na pia kitu kingine cha msingi alijitahidi kuwasoma
personality zao..
Baada
ya kumaliza kufanya ‘tafiti’ zake Carl alienda hatua ya pili ya
maandalizi ambapo ilikuwa ni kuandaa ‘makazi na stoo’ yake ya muda
katika msitu uliopo karibu na bank ambapo alichimba handaki dogo kwa
ustadi mkubwa na kulificha kabisa kwa juu mtu asiweze kujua kwa namna
yoyote ile..
Moja
ya wapelelezi ambao walihusika kufanikisha kumkamata Carl anaeleza Bw.
Carr anaeleza kuwa siku ambayo walifanikiwa kugundua na kuliona handani
mojawapo ambalo lilichimbbwa na Carl walistaajabu (kumbuka Carl alikuwa
na zaidi ya mahandaki 30 sehemu tofauti tofauti za nchi ya marekani)!
Inaelezwa
kuwa kinachostaajabisha kuhusu mahandaki ya Carl ni jinsi yalivyo
chimbwa kiustadi na kujengewa kwa ndani kwa vitofali vidogo vidogo.. Pia
handaki lilikuwa linampangilio wa hali ya juu wa kiwango cha kijeshi
(military precision).
Ndani
ya handaki kulikuwa na kila kitu ambacho angekihitaji, silaha, nyaraka
za ‘research’, kifurushi cha kujikimu (survival kit), madawa ya dharura
(first aid kit), vinyago vya kuficha sura (masks), fedha taslimu,
majarida ya mazoezi ya kawaida na kijeshi na vitu vingine vingi..
Baada
ya kumaliza maandalizi haya ya msingi Carl alijichimbia katika maktaba
ya umma ya Philadelphia ambapo ndio alipafanya kama ofisi yake kwani
inaelezwa kuwa alikuwa na mazoea ya kutumia muda mwingi hapo akifanya
‘tafiti’ na angekuwa hapo kwa wiki kadhaa ili ku-fainalize mpango wake
na kufanya conclusion ya jinsi atakavyotekeleza tukio lenyewe..
UTEKELEZAJI WA TUKIO
Matukio yote ambayo Carl aliyafanya alikuwa anayetekeleza mwezi October au November ambapo maeneo mengi yanakuwa yapo kwenye kipindi cha winter au autumn ambapo kunaambatana na baridi kali pamoja na jua kuzama mapema! Pia matukio yake yote aliyatekeleza siku ya ijumaa na hii ndio iliyomfanya apewe jina la ‘The Friday Night bank robber’..
Matukio yote ambayo Carl aliyafanya alikuwa anayetekeleza mwezi October au November ambapo maeneo mengi yanakuwa yapo kwenye kipindi cha winter au autumn ambapo kunaambatana na baridi kali pamoja na jua kuzama mapema! Pia matukio yake yote aliyatekeleza siku ya ijumaa na hii ndio iliyomfanya apewe jina la ‘The Friday Night bank robber’..
Uchaguzi
wake wa muda wa kufanya tukio ulimpa advantage kadhaa.. Kwanza kipindi
cha winter na autumn jua linazama mapema kwa maana ya kwamba katika
masaa yale yale ambayo bank zinakuwa zinafungwa lakini katika kipindi
hiki cha majira ya mwaka giza linakuwa limeanza kuingia hivyo inampa
mwanya mzuri kufanya tukio.. Pia kufanya tukio ijumaa ilimaanisha kuwa
ndio siku nzuri kwa bank kuwa na kiwango kikubwa cha Cash.
.
Lakini
pia alitumia sababu ya kisaikolojia kuwa ijumaa wafanyakazi wanakuwa
distracted kutokana na weekend kuanza hivyo umakini unakuwa mdogo..
Kwahiyo alichokifanya Carl kwanza ni kupaka ‘harufu’ kwenye nyumba zote
zilizo karibu na bank ili kuwachanganya mbwa wa polisi wakija kujaribu
kutafuta trail ya alikoelekea!
Sasa
basi, siku ambayo Carl alikuwa anafanya tukio alivaa kinyago cha
kutisha usoni ambacho kili-fit sawa sawa kabisa ili kuficha ngozi yake
na! Pia alivaa manguo mengi ili kuleta muonekano kwamba ni mnene.. Na
alikuwa akiingia ndani ya bank alitembea dizaini kama amechuchumaa mfano
wa Kaa (crab)! Vitu vyote hivi alivyovifanya watu walihisi labda
alikuwa na matatizo ya akili lakini hawakujua kuwa alivifanya kwa kusudi
kabisa..
Alivaa
kinyago cha kutisha ili kuleta effect ya kuogofya na kuficha tone ya
ngozi yake, pia alivaa manguo mengi ili kuficha body size, na alitembea
kama kaa akiwa kama amechuchumaa ili kuficha height!! Hii ilimsaidia
sana kwani kwa miaka 30 FBI walishindwa kung’amua mtu wanayemtafuta
alikuwa wa size gani, height gani au skin color ipi???
Carl
alikuwa anasubiri dakika 5 kabla bank haijafungwa ndipo alikuwa
anavamia! Hii ilimpa possibility nzuri kuwa ndani kulikuwa na wafanya
kazi pekee au Wateja wachache sana wamebakia
Akishavamia
bank alitoa bastola na kuamuru watu walale chini na wasimuangalie!
Mashahidi wanaeleza kuwa kwa ustadi mkubwa (labda kutokana na mazoezi ya
karate) Carl aliruka kutoka alipo mpaka kwenye droo za ma-teller na
kuweka fedha zote alizozikuta humo kisha kwa ustadi ule ule aliruka tena
mpaka upande wa wateja na kuwaamuru tena kwa msisitizo wasimuangalie na
kabla hawajang’amua kinachoendelea Carl alikuwa tayari ashatoka nje ya
bank na kutokomea katika msitu ulio karibu.
Inaelezwa
kuwa katika matukio yake yote aliyatekeleza ndani ya muda usiozidi
dakika mbili! Yani chini ya dakika mbili alikuwa tayari amevamia,
amekomba hela na ameshatokomea msituni..
Carl
anaeleza mwenyewe kuwa akiingia ndani ya msitu alikuwa anakimbia kwa
dakika kadhaa kama kumi hivi mpaka mahala ambapo anakuwa ameficha
baisikeli kisha anaendesha mpaka ndani ndani kabisa ya msitu kulipo na
handaki lake, akifika kwenye handaki kila kitu anakiacha hapo; fedha
alizoiba, masks, nguo, gloves etc kisha anavaa nguo nyingine za kawaida
anaendesha baisikeli anaondoka!
Carl
anasema kuwa ataendesha baisikeli kwa muda wa kama dakika ishirini au
zaidi mpaka upande wa pili wa msitu ambapo kuna barabara na hapo
kunakuwa kuna gari amepaki linamsubiri.. then anawek baisikeli ndani ya
gari anaendesha kama raia wa kawaida na kuelekea nyumbani..
Carl
anasema alikuwa anacha wiki au miezi ipite mpaka stori kuhusu tukio la
ujambazi zianze kufifia ndipo anarudi kwenye ule msitu na kuchukua ‘hela
zake’… Baada ya hapo maisha yanaendelea na anaanza ‘tafiti’ kwa ajili
ya tukio linalofuata..
KUKAMATWA NA MAZINGAOMBWE YA HUKUMU
Kukamatwa kwa Carl kulikuwa kwa bahati mbaya mno! Kuna watoto walikuwa wanacheza katika msitu uliopo karibu na nyumbani kwao! Wakiwa ndani ya huo msitu waliokota PVC tube/pipe iliyokuwa imefichwa..
Kukamatwa kwa Carl kulikuwa kwa bahati mbaya mno! Kuna watoto walikuwa wanacheza katika msitu uliopo karibu na nyumbani kwao! Wakiwa ndani ya huo msitu waliokota PVC tube/pipe iliyokuwa imefichwa..
Baada
ya kuifungua ndani walikuwa ilikuwa na bastola na vitu vingine kadhaa
vinavyotia shaka. Wale watoto wakawataarifu wazazi wao na wazazi wao
wakashauri vipelekwe polisi!
Baada
ya vitu hivyo kupelekwa polisi, vikachunguzwa na kukakutwa ramani..
Polisi walipoifuatilia ile ramani ikawqpeleka moja kwa moja kwenye
handaki dogo ndani ya msitu! Kutokana na vitu vilivyokutwa ndani ya
handaki hilo polisi wakapata wasiwasi kuwa inawezekana wanadeal na ishu
serious kuliko uwezo wao hivyo wakawataarifu FBI!
Baada
ya FBI kuwasili iliwachukua masaa kadhaa tu kung’amua kuwa vitu hivyo
vinahusiana moja kwa moja na Jambazi wanayemtafuta kwa miaka 30, The
Friday night bank robber. FBI walitumia alama za vidole walizozikuta
kwenye ile handaki na pia walitumia kijarida kidogo kinachohusu kituo
cha mafunzo ya karate kumtrack down Carl mpaka wakampata. Siku Carl
anakamatwa alikutwa “ofisini kwake” Maktaba ya Philadelphia Free Library
akiwa anafanya “tafiti”
Baada
ya kukamatwa na kesi kufikishwa mahakamani ilikuwa ni dhahiri kuwa Carl
atahukumiwa kifungo cha maisha au aghalabu miaka 115 pasipo uwezekano
wa kupata parole kutokana na mashitaka yanayomkabili
Lakini
mwisho wa siku Carl alikubaliana deal na FBI kuwa awaeleze nukta kwa
nukta kuhusu matukio yote 50 aliyoyafanya, pia akubali kushirikiana na
FBI kutengeneza programu maalum kuwasaidia maafisa wa FBI kutambua namna
ya kuwabaini ‘serial criminals’, na pia awaelekeze kuhusu saikolojia ya
ku-plan matukio ya uhalifu yaliyo perfect.!
Carl
akakubaliana na masharti yote haya na mahakama ikapunguza adhabu yake
kutoka kifungo cha maisha mpaka kifungo cha miaka 17 bila parole..
Hivyo
basi ikifika 2021 Carl Gugasian anarudi uraiani! Inaelezwa kuwa huko
gerezani Carl ni mtu mnyoofu mno na ni mfungwa wa kuigwa na ameendeleza
desturi yake ya kupenda mazoezi hivyo yuko katika afya njema sana na
wengi wanaamini atafika 2021 akiwa salama salimini.