Makamu Mwenyekiti wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Nassor Idrissa, amepanda cheo na kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo.
Idrissa
anachukua nafasi ya aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo Alhaji Said
Mohamed Abeid, aliyefariki dunia mwanzoni mwa mwezi huu.
Kwa
mujibu wa barua iliyoandikwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad
Kawemba, na kuituma kwenda kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
kuwafahamisha mabadiliko hayo, imeeleza kuwa Shani Christoms Mligo,
ndiye atakuwa Makamu Mwenyekiti mpya wa timu hiyo akichukua nafasi ya
Idrissa.
Mabadiliko
hayo ya kiuongozi yamefanywa na Bodi ya Wakurugenzi ya Azam FC, ambapo
uteuzi huo umeanza rasmi leo Novemba 29 mwaka huu.