Stiker Ismail Mrisho amefariki dunia uwanjani wakati
akiitumikia klabu yake ya Mbao FC U20 dhidi ya Mwadui FC, taarifa kutoka
mjini Bukoba zinasema kijana huyo atazikwa leo jioni nyumbani kwao
jijini Mwanza.
Mwili wa marehemu tayari umeshasafirishwa kwenda jijini Mwanza ambako
ndipo nyumbani kwao maremu. Msiba utakua eneo la Dampo karibu na chuo
cha Mount Meru huku mazishi yakitarajiwa kufanyika leo majira ya saa 10
jioni.
Mechi zote za kituo cha Bukoba ambazo zilikuwa zinatarajiwa kuchezwa leo zimeahirishwa kupisha msiba huo.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka mjini Bukoba, Serikali ya mji
huo imetoa gari la wagonjwa (ambulance) ambalo limebeba mwili wa marehem
kuusafirisha kwenda Mwanza.
Monday, 5 December 2016
About Unknown
Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.