Beki Virgil van Dijk rasmi ameanza mazoezi Liverpool akiwa amevaa kwa mara ya kwanza jezi ya klabu hiyo mazoezini.
Van Dijk amesajiliwa kutoka Southampton kwa kitika kikubwa cha pauni milioni 75 na kusababisha gumzo kubwa.
Beki
huyo mwenye umri wa miaka 26, ameanza mazoezi ya fitnesi akiwa na
kitengo cha fitnesi cha benchi la Liverpool ambacho lazima kijiridhishe
kabla ya kumkabidhi kwa Kocha Jurgen Klopp ili amtumie.