Fashion

Sunday 7 January 2018

CHIRWA MWENDO WA MAHINDI HUKO ZAMBIA

 
Kamati ya nidhamu ya klabu ya Yanga, italazimika kukaa leo kumjadili mshambuliaji wake Obrey Chirwa.

Chirwa ambaye tayari yuko nchini baada ya kujichimbia kwao Zambia, analazimika kujadiliwa na kamati hiyo ambayo itatoa uamuzi.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinaeleza, kamati hiyo itatoa uamuzi wa adhabu au la baada ya kujadili.

“Chirwa hawezi kwenda Zanzibar kwa sasa hadi hapo kamati itakapojadili na kutoa jibu. Kama hana adhabu atakwenda Zanzibar kama ana adhabu hatakwenda,” kilieleza chanzo.


Chirwa aliweka mgomo wa kurejea mapema kwa madai ya kumaliziwa fedha zake za usajili jambo ambalo hata hivyo, uongozi wa Yanga haukupenda lizungumwe sana.

Unknown

About Unknown

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :