Mshindi pekee wa tuzo ya
Ballon D’Or kutoka katika bara la Afrika George Weah ameshinda kiti cha
uraisi nchini Liberia katika kura zilizohesabiwa.
George Weah nyota wa zamani wa Ac Millan ameshinda katika majimbo 12
kati ya majimbo 15 nchini humo akimshinda mpinzani wake wa karibu sana
Joseph Boakai.
Joseph Boakai mwenye umri wa miaka 73 amekuwa makamu wa raisi nchini
Liberia kwa muda wa miaka 12 sasa lakini hiyo haikutosha kumpa ushindi
kwani aliambulia ushindi majimbo mawili tu.
Weah amewahi kushinda tuzo ya mchezaji bora Africa mara 3, kombe la
Serie A mara 2, Ligue 1 mara 1, FA Cup mara 1 na Ballon D’Or 1 tuzo
ambayo hadi sasa hakuna Muafrika mwingine ambaye kaichukua