Mchakato wa kupata kocha wa timu ya taifa ya Uganda na namna ambavyo wenzetu walivyokuwa makini pindi linapokuja suala linalohusu timu zao taifa, mchakato huu ulihusisha hadi wataam kutoka nje ya nchi.
Hapa unamzungumzia mtu kama Kalusha Bwalya ambaye historia yake katika soka la Afrika hakuna mtu ambaye haifahamu.
Kuhusika kwa Bwalya katika mchakato wa kumpata kocha wa timu ya taifa ya Uganda maana yake ni kwamba, Uganda walikuwa wanahitaji mtu sahihi wa kuifundisha timu yao.
Walihitaji mtu mwenye jicho la kiufundi kwa ajili ya kuwashauri ni kocha gani atawafaa kati ya wote waliotuma maombi kuhitaji nafasi hiyo.
Sébastien akiwa na umri wa miaka 41 lakini pia ana uzoefu na soka la bara la Afrika, tayari ameshawahi kufundisha vilabu kama Esparance Sportive de Tunis ya Tunisia, Wydad Athletic Club, CRD Libolo pamoja na ACEC Mimosas kwa nyakati tofauti.
FUFA kwa kutambua kwamba makocha wazawa wanahitajika, wanampeleka kusoma nchini Marekani halafu baada ya hapo atafanya program maalum ambayo imeandaliwa na chama hicho cha soka nchini Uganda kwa lengo la kuendeleza mpira wa miguu nchini humo. Kwa hiyo Basena ambaye alikuwa kocha wa muda tangu kuondoka kwa Micho, bado yupo kwenye mfumo wa FUFA.