Mtanzania Mbwana Samatta amethibitisha kuwa hajaenda Ulaya kushangaa baada ya kuifungia timu yake ya KRC Genk bao wakati ikishinda 4-0 katika play off ya kwanza dhidi ya KV Oostende nchini Ubelgiji.
Samatta anayevaa jezi namba 77 alifunga bao hilo katika dakika ya 77 ikiwa ni dakika chache baada ya kuingia uwanjani.
Ushindi huo kwenye dimba lao la nyumbani la Cristal Arena linaifanya Genk kujiweka katika mazingora mazuri katika mechi ya marudiano.
Mabao mengine ya Genk yalifungwa na Alejandro Melero katika dakika tya 12, Thomas Buffel akafunga katika dakika ya 21 na wakaenda mapumziko wakiwa mbele.
Kipindi cha pili, Samatta akaanza kufanya yake kabla ya Neeskens Kebano kufunga bao la nne katika dakika ya 85.