Fashion

Wednesday 27 April 2016

YANGA NA MGAMBO MPAKA SASA GOLI NI MOJA KWA MOJA

Dakika ya 37: Mchezo unaendelea
 
Dakika ya 35: Mchezo umesimama, kipa wa Mgambo kaumia.

Dakika ya 34: Mvua imekatika, timu zote zinashambuliana kwa zamu, mpira umemilikiwa zaidi na viungo wa timu zote.

 

Dakika ya 30: Msuva anakatwa ndani ya eneo la hatari la Mgambo lakini mwamuzi anapeta.

Dakika ya 27: Salum Telela anapewa kadi ya njano kutokana na kucheza faulo.

Dakika ya 26: Mgambo wanaendelea kuwa wagumu kukubali ngome yao kupitika.

Dakika ya 23: Mchezo unaendelea.

Juma Abdul ilionyesha kuwa na maumivu na alitoka akiwa anachechemea.

Dakika ya 21: Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Juma Abdul anaingia Mbuyu Twite.

Dakika ya 21: Kipa wa Mgambo, Said Hamis ameumia na yupo chini, mchezo umesimama.

Dakika ya 19: Mgambo wanafanya shambulizi lakini inakuwa offside.

Dakika ya 15: Mgambo wanazuia vizuri lango lao kutokana na Yanga kuonekana kutafuta bao kwa nguvu.

Dakika ya 10: Yanga wameamka na kuanza kushambulia lango la Mgambo. 

Bao hilo limefungwa dakika ya 4, mfungaji ni Bolly Ajaly

Dida alimuanzishia mpira Telela ambaye alishindwa kuumiliki na kujikuta akinyang'anywa na washambuliaji wa Mgambo ambao walitumia nafasi hiyo kutupia mpira wavuni

Mgambo wanapata bao kutokana na uzembe wa kiungo wa Yanga, Salum Telela.


Dakika ya 3: Timu zote zinacheza mchezo wa kusomana, mchezo bado haujachangamka.


Mchezo umeanza


Timu ndiyo zinaingia uwanjani kwa ajili ya kuanza mchezo.


Idadi ya watu siyo wengi sana uwanjani kutokana na mvua kunyesha jijini Dar es Salaam, mpaka sasa kuna manyunyu eneo hili la Uwanja wa Taifa.


KIKOSI CHA YANGA:
Deogratius Munish ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Kelvin Yondani, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Salum Telela, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Paul Nonga, Amissi Tambwe, Deus Kaseke.

WANAOANZIA BENCHI
Benedict Tinocco, Mbuyu Twite, Vincent Bossou, Matheo Anthony, Donald Ngoma, Thaban Kamusoko, Mwinyi Hajji.

 
KIKOSI CHA MGAMBO:
Said Hamis, Salum Mlima, Chande Magonja, Henry Chacha, Bakari Mtama, Salum Kipanga, Nassor Gumbo, Mohammed Samatta, Herbert Lukindo, Bolly Ajaly, Salum Gila.

WANAOANZIA BENCHI
Mudathir Hamis, Bushiru Mohammed, Francis, Anyosisye, Ally Nassoro, Nurdin Mkomeni, Uda Bakari, Abuu Daud.


Timu zote zimeshaingia uwanjani kupasha misuli, wachezaji wote watakaoanza na wale wanaoanzia benchi.

Unknown

About Unknown

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :