Fashion

Friday, 30 December 2016

NGASSA KUANZA KANDARASI YAKE MBEYA CITY


Klabu ya Mbeya City sasa itakuwa na ruhusa ya kumtumia mshambuliaji wake Mrisho Ngassa, wakati ligi itakapoendelea kwa mzunguko wa 19, baada ya timu ya  Fanja ya Oman kutuma Hati yake ya Uhamisho wa Kimataifa ITC.


Mwenyekiti wa Mbeya City, Mussa Mapunda amesema leo kwamba ITC ya Ngassa imefika nchini asubuhi ya leo na sasa mchezaji huyo atakuwa huru kuanza kuichezea timu yao kwenye mchezo ujao dhidi ya Azam ambao umepangwa kupigwa Januari 16.

Mapunda amesema kwamba anawashukuru Fanja, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Chama cha Soka Oman (OFA) ambao kwa pamoja wamefanikisha kupatikana kwa ITC hiyo.

“Ni kweli tumeipata, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Shirikisho la Soka nchini, TFF, Chama cha Mpira cha Oman, hakika wamefanya kazi kubwa kufanikisha kupatikana kwa ITC  hii na pia naishukuru Fanja FC na watendaji wote kwenye timu yetu, tumekuwa na mawasiliano mazuri muda wote mpaka tumefanikiwa,” amesema. 

Mapunda amesema kwamba kuchelewa kufika kwa ITC hiyo hakukuwa na msuguano wowote baina ya klabu hizo mbili, bali kilichokuwa kinatokea ni tofauti ya wakati na siku za ufanyaji kazi  kwenye ofisi kulingana na taratibu za nchi hizo mbili, yaani Oman na Tanzania.
“Hakukuwa na msuguano wowote uliosababisha kuchelewa kwa ITC  hii, kilichokuwepo ni utofauti wa taratibu za kiofisi, mara nyingi Oman siku za Ijumaa na Jumamosi inakuwa ni mapumiko na huku kwetu Jumapili inakuwa mapumziko,”amesema.

Unknown

About Unknown

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :