Timu ya Simba inamtaka beki wa kulia wa Prisons, Salum Kimenya na hii si
mara ya kwanza, sasa wanavutana kwani beki huyo anataka dau la Sh
milioni 80 lakini Simba inazo Sh milioni 30 tu. Wamekwamia hapo.
Mabeki
wa zamani wa Simba na Yanga, Boniface Pawasa na Bakari Malima wameipa
Simba mchongo kuwa, kama wakimpata beki huyo mambo yao yatakuwa mazuri
hata kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Ni
hivi, Simba inataka kumaliza tatizo la beki wa kulia kwani ina mpango
wa kumtumia Janivier Bokungu kama beki wa kati kutoka kulia japokuwa
taarifa zaidi zinasema pia inaweza kumtema mkabaji huyo.
Kimenya
yeye anasisitiza kuwa ni mwajiriwa wa Jeshi la Magereza hivyo ili
ajiunge na Simba ni lazima aiteme ajira yake ndiyo maana anataka dau la
Sh milioni 80 vinginevyo hawezi kuchezea ajira yake.
Akizungumza
na Kimenya alisema; “Unajua mimi hapa Prisons nipo kwenye ajira, siwezi
kuacha kazi yangu kwa Sh milioni 30 yaani nitakuwa nimefanya kosa kubwa
sana.
“Sitaki
yanikute yaliyowakuta baadhi ya wachezaji walioacha kazi hapa na kwenda
kujiunga na hizo timu, naweza kuacha kazi halafu huko nikakaa msimu
mmoja, unaofuata nikafungashiwa virago, sasa nitakuwa nimefanya nini?
“Kama Simba wananitaka kweli wanipate fedha nzuri nikawafanyie kazi ambayo wataridhika nayo,” alisema Kimenya.
Wakizungumza
kwa nyakati tokfauti, beki wa zamani wa Simba, Boniface Pawasa na yule
wa Yanga, Bakari Malima walisema kuwa kama kweli Simba wana nia ya
kumsajili Kimenya basi wafanye kweli kwani atawasaidia kwa kiasi
kikubwa.
“Binafsi
namjua vizuri sana Kimenya, nimekuwa nikimfuatilia kwa karibu sana, ni
mchezaji mzuri ambaye uchezaji wake ni kama wa Shadrack Nsajigwa, siyo
mtu wa kutaka tamaa pia ni mpambanaji anayetaka ushindi muda wote,”
alisema Pawasa ambaye pia ni mchambuzi wa michezo katika gazeti la
Championi.
Kwa
upande wake Malima ambaye pia ni mchambuzi katika gazeti hili, alisema:
“Kimenya ni beki mzuri pia ana uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani,
kama Simba wanataka kumsajili, binafsi nawashauri wafanye kweli
atawasaidia sana.”
Simba wamekuwa wakifanya siri kuhusu mipango yao ya kumsajili Kimenya ambaye anamaliza mkataba mwishoni mwa msimu huu.
SOURCE: CHAMPIONI
10
Dec
2016