Yanga kwa mara ya kwanza ikiwa chini ya Kocha George
Lwandamina, leo Jumamosi inacheza mechi ya kirafiki na JKU ya Zanzibar
kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Mbali
ya Lwandamina aliyechukua nafasi ya Hans van Der Pluijm, Yanga pia
itacheza kwa mara ya kwanza kikosini ikiwa na kiungo Justine Zullu na
kocha msaidizi Noel Rodwell Mwandila.
Meneja
wa Yanga, Hafidh Saleh ameliambia Championi Jumamosi kuwa, wamefanya
mazoezi kwa wiki mbili na sasa ni wakati wa kutazama kile walichofanya.
“Kikosi
kipo vizuri na maandalizi yote ya mechi hii yapo sawa, tunataka kupima
kikosi chetu tunaomba mashabiki wetu waje wengi kutazama kikosi chao
kipya,” alisema Saleh.
Yanga
inacheza mechi hii ikiwa imesaliwa na siku tano za kufanya usajili huku
ikielezwa kupanga kutumia mchezo huo kumuaga mchezaji wake kiraka
aliyemaliza mkataba Mbuyu Twite.