Fashion

Wednesday, 11 January 2017

NAPE AMKABIDHI BENDERA DIOMOND KUELEKEA GABON




Katika kuhakisha wanafanikisha shoo msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul 'Diamond Platinum' kwenye ufunguzi wa Afcon, Kampuni ya Multichoice kupitia king'amuzi cha DStv imetoa tiketi sita kwa vijana wake watakaokwenda nchini Gabon katika ufunguzi huo.

Ufunguzi huo wa michuano hiyo mikubwa Afrika, inatarajiwa kufanyika Januari 14, mwaka nchini huko ambako Dimaond amealikwa kwenda kutuimbuza.
 


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alimkabidhi bendera ya taifa, Diamond kwa ajili ya kwenda kuipeperusha vyema Tanzania katika ufunguzi huo.
 


"Kikuweli nimpongeze Diamond kwa mwaliko alioupata wa kwenda kutumbuiza kwenye michuano mikubwa Afrika ya Afcon, siyo kitu kidogo kwake, ni nafasi ya yeye kujitangaza zaidi kimataifa, ninaamini wapo wasanii wengi wazuri Afrika, lakini kachaguliwa yeye hivyo anastaili pongezi," alisema Nape.

Nape ndiye aliwaomba DStv kujitokeza na kudhamini safari ya wachezaji shoo wa Diamond na baadhi ya watu wa timu yake kwenda Afcon ili kuhakikisha anafanya shoo ya uhakika zaidi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa DStv, Salum Salum alisema wametoa tiketi hizo kwa Diamond kwa lengo kukuza na kuendeleza vema tasnia ya filamu.

"Tunathamini tasnia ya sanaa nchini kwa kupitia muziki na filamu, hivyo basi katika kutambua hilo tumetoa tiketi sita kwa kundi la WCB chini ya msanii Dimaond kwa ajili ya kwenda kwenye uzunduzi wa Afcon huko Gabon.

Tumempatia tiketi hizo, baada ya kuomba udhamini wa tiketi hizo kwa ajili ya vijana wake sita atakaombatana nao kwenye shoo hiyo na kikubwa tunataka kuona Diamond anafunika ili atauwakirishe vema," alisema Salum.

DStv, ndiyo itaonyesha michuano hiyo mikubwa ya kimataifa kwa kifurushi chake cha bei cha chini kabisa kitakachopatikana kwa Shilingi 19, 975 tu.

Unknown

About Unknown

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :