Fashion

Friday, 6 January 2017

REHEMA MADUSA BEGA KWA BEGA NA WANANCHI KULETA MAENDELEO CHUNYA


Katika hali ya kuhakikisha Wilaya ya Chunya inapiga hatua katika nyanja mbalimbali Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa ameamua kuhama ofisini kwake na kuungana na wananchi wa Wilaya hiyo ili kukamilisha Miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.


Hivi karibuni Madusa amefanya ziara katika kijiji cha Itumbi Mamlaka ya Mji mdogo wa Makongolosi ambapo alikagua mradi wa Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji hicho ambapo wananchi wanalazimika kutembea umbali wa kilometa zaidi ya kumi tano hadi kijiji jirani cha Matundasi ili kupata huduma ya Afya hali inayowapa kadhia kubwa hasa akina mama wajawazito ambapo hutumia usafi hatari wa pikipiki ambapo hugharamia pesa nyingi na wasio na uwezo hupoteza maisha.


Mradi huu unajengwa kwa nguvu za wananchi wa Itumbi na wadau wa maendeleo.
Madusa amesema Serikali inaunga mkono juhudi za wananchi na kuwataka wakamilishe mradi huo ifikapo mwezi juni mwaka huu.


Aidha Mkuu wa Wilaya akiwa ameambatana na Kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Chunya alikagua mradi wa Ujenzi wa vyoo vya shule ya msingi Itumbi ambapo amefurahishwa na ujenzi wa vyoo hivyo ili kuwaondolea adha ya msongamano wa wanafunzi katika vyoo.


Amewataka wananchi kuongeza kasi ili vyoo hivyo vikamilike katika kipindi kisichozidi zidi wiki mbili ili kutimiza agizo la Rais John Pombe Magufuli la kuwataka wananchi kujenga vyoo kwa kufuata utaratibu wa wavulana ishirini na tano kwa tundu moja na wasichana ishirini kwa tundu. 


Madusa amesema linapokuja suala la maendeleo mambo ya siasa yawekwe kando kwani pindi yanapotokea magonjwa hayataangalia huyu ni wa chama gani.


Hata hivyo amewataka wananchi waliopo nje ya Wilaya hiyo kuelekeza nguvu zao maeneo wanayotoka kwani pindi wakirudi wanafaidika na huduma hizo.

Unknown

About Unknown

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

2 Maoni yako

Write Maoni yako