Baada
ya kufunga mabao manne wakati Tottenham ikiitwanga Leicester kwa mabao
6-1, sasa vita mpya ya wafungaji bora katika Ligi Kuu England.
Kane
sasa amefikisha mabao 26 akiwavuka Romelu Lukaku wa Everton ambaye
alikuwa akiongoza akiwa na mabao 24, sasa yuko nafasi ya pili na nafasi
ya tatu ni Alexis Sanchez wa Arsenal mwenye mabao 23.