Manchester United wameifunga Real Madrid kwa mikwaju ya penalti baada ya kumaliza dakika 90 kwa sare ya goli 1-1.
Casemiro aliisawazishia Madrid kwa njia ya penalti baada ya mlinzi mpya wa United Victor Lindelof kumuangusha Theo Hernandez katika eneo la hatari.
Penalti saba kati ya kumi hazikuingia nyavu
Haukuwa usiku mzuri kwa Lindelof ambaye aliendeleza makosa yake na kukosa mkwaju wa penalti.
United wameshinda michezo yote minne katika ziara nchini Marekani na watakutana na Barcelona katika fainali siku ya Jumatano.