Beki huyo anaamini Simba itashinda kwa namna yoyote kwani wachezaji waliomo kwenye kikosi hicho wana uchu wa kuifunga Yanga na uwezo wao ni mkubwa.
Kapombe ambaye mara kwa mara amekuwa akisumbuliwa na tatizo hilo, hivi karibuni alijitonesha alipokuwa akiitumikia timu ya Tanzania, Taifa Stars dhidi ya Rwanda kwenye mchezo wa kusaka tiketi ya kushiriki Michuano ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN).
Kapombe amesisitiza kuwa mchezaji wa leo ni ushindi wao: “Kwa sasa naendelea vizuri kwani yale majeraha yangu yamepona na sisikii maumivu, muda wowote naweza kuungana na wenzangu kwa ajili ya mazoezi ya kujiandaa na msimu ujao, kuhusu mchezo wa leo wa Ngao ya Jamii hakika nina imani na wachezaji wenzangu watatuwakilisha kwa ushindi.
“Sifurahii kukaa nje, nimekuwa nikipambana kuhakikisha napona haraka na kurejea uwanjani kuipambania timu yangu, kitu cha faraja ni kwamba kwa sasa naweza kufanya hivyo kutokana na kupona kwangu hivyo mchezo wa leo sina hofu kwani timu yangu ina uwezo wa kushinda bila mimi,” alisema Kapombe.