Fashion

Sunday, 13 August 2017

KOFI ANNAN AMPA SOMA ODINGA


 
Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan, ambaye alikuwa mpatanishi mkuu baada ya mzozo wa kisiasa nchini Kenya miaka kumi iliyopita, ametoa wito kwa walioshindwa kutumia mifumo ya kisheria kutafuta haki
.

Bw Annan alikuwa mpatanishi mkuu baada ya ghasia kuzuka baada ya uchaguzi mkuu wa 2007 uliokumbwa na utata.

Bw Mwai Kibaki alitangazwa mshindi wakati huo lakini Bw Raila Odinga na chama chake cha ODM wakapinga matokeo hayo.

Katibu mkuu huyo wa zamani wa UN amempongeza Bw Kenyatta kwa ushindi wake na pia akamsifu Bw Odinga kwa kuendesha kampeni yake kwa njia ya amani.

"Namshukuru kiongozi wa upinzani Raila Odinga kwa kampeni ya uchaguzi ya amani aliyoiendesha. Amekuwa mtetezi jasiri wa demokrasia," amesema Dkt Annan kupitia taarifa.

"Kwa hivyo, namhimiza sasa afuatilie malalamiko yake kupitia mifumo ya kisheria iliyowekwa na aweke maslahi ya taifa mbele, kama alivyofanya kwa uzalendo mara nyingi awali."

Upinzani umekuwa ukidai mitambo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) ilidukuliwa na matokeo kuchakachuliwa kumfaa Rais Kenyatta.

Alhamisi, muungano wa upinzani National Super Alliance (NASA) ulidai Bw Odinga ndiye aliyeshinda uchaguzi huo na kuitaka tume hiyo kumtangaza kuwa mshindi.

Rais Kenyatta alipata kura 8, 203, 290 ambayo ni asilimia 54.27 naye mpinzani wake mkuu, mgombea wa muungano wa upinzani wa National Super Alliance Raila Odinga akapata kura milioni 6,762,224 ambayo ni asilimia 44.74.

Maajenti wakuu wa NASA waliondoka ghafla kikao cha tume hiyo cha kuafikiana kuhusu matokeo hayo kabla ya kutangazwa kwa Bw Kenyatta kuwa mshindi wa uchaguzi huo Ijumaa usiku

Unknown

About Unknown

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :