Wednesday, 23 August 2017
YANGA KAFA KWENYE MATUTA KWA 4-5 TAIFA
DAKIKA 90 ZIMEKAMILIKA, SASA NI MKWAJU YA PENALTI
Dk 90+2 Niyonzima anamchambua Gadiel, anaachia mkwaju mkali kabisa lakini juuuuuuuu
Dk 90+2 Gadiel anafanya kazi ya ziada, anaokoa na kuwa kona, inachongwa na Yanga wanaokoa
Dk 90+1, Simba wanapata kona hapa, inachongwa na Kichuya lakini mpira unakwenda nje, goal kick
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 90 Simba wanaendelea kumiliki mpira lakini hawana malengo yanayotimia langni mwa Yanga ambao wako makini kiulinzi
SUB Dk 88, Mohamed Zimbwe Jr, anaingia kuchukua nafasi ya Nyoni ambaye ameumia
Dk 88 sasa, Nyoni yuko chini pale anatibiwa, mchezo umesimama
SUB Dk 87, Yanga wanamuiginza Hassan Kessy anaingia kuchukua nafasi ya Juma Abdul
KADI Dk 87 Yondani analambwa kadi ya njano hapa
Dk 85 sasa, Simba ndiyo wamemiliki mpira kwa muda mrefu zaidi lakini wajanja kuipita ngome ya Yanga
Dk 81, Mo Ibrahim, lakini kipa wa Yanga anafanya kazi kubwa kuokoa mpira huo, anamgonga Vicent, yuko chini
anatibiwa
Dk 80, Simba wanapata kona, inachongwa, Kichuya anajaribu lakini Yanga wanaokoa
Dk 79 Martin anaingia na kuachia mkwaju mkali, Manula anaokoa lakini mwamuzi anasema ilikuwa faulo
SUB Dk 78 Mohamed Ibrahim anaingia kuchukua nafasi ya Muzamiru
Dk 77 Tshishimbi ameachia shuti kali hapa lakini hakulenga lango
Dk 76, umbali wa takribani mita 25 lakini hakulenga lango
Dk 75, Gadiel anatoka katika nafasi yake, anafanya kazi ya ziada na kuokoa mpira miguuni kwa Liuzio ambaye kama angepiga, yangekuwa mengine
SUB Dk 73 Juma Mahadhi anaingia kuchukua nafasi ya Raphael Daud
SUB Dk 72 Juma Liuzio anaingia kuchukua nafasi ya Mavugo upande wa Simba
Dk 72, Martin anaachia krosi safi kabisa langoni mwa Simba, lakini hakuna mtu
Dk 69 sasa, mpira umebaki katikati mrefu na inaonekana kutakuwa na shambulizi la kushitukiza upande mmoja litakalozua madhara
Dk 65, Yanga wanafanya shambulizi la kushitukiza, mabeki wa Simba wamezidiwa ujanja, lakini Manula anatoka na kuokoa
Dk 62, Ajibu anamfanyia madhambi Shomari, mwamuzi anampa onyo kwa mdomo tu akimsisitiza kutulia
Dk 60, mechi bado inaonekana haina spidi kali kama ambavyo ilitarajiwa. Lakini Yanga wanaonekana kuna kitu wanatafuta na hasa kwa shambulizi la kushitukiza kwa kuwa wanajaza wachezaji wengi nyuma kwa ulinzi na Simba wanaonekana kujisahau mara kadhaa
Dk 56, Okwi anamzidi kasi Yondani, anabaki yeye na kipa lakini Kipa Mcameroon anafanya kazi nzuri kabisa, anaokoa miguuni mwa Okwi
Dk 53, Kamusoko anaachia mkwaju mkali kwelikweli lakini unapita juu ya lango Simba, angelenga ingekuwa hatariiii
KADI DK 50, Kadi ya tatu ya mchezo, Niyonzima analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Juma Abdul aliyempokonya mpira
Dk 48, krosi fupi ya Nyoni, Mavugo anaruka peke yake na kupiga kichwa safi lakini Goal Kick
Dk 47, Okwi anaachia mkwaju mkali hapa lakini gadiel anaokoa na kuwa kona, inachongwa na kuokolewa
DK 46, Juma anamimina krosi safi kabisa lakini kipa Manula anadaka vizuri kabisa
Dk 45, Mechi imeanza na Simba wanafanya shambulizi kali, Okwi anaingia lakini Youthe anaokoa vizuri kabisa hapa
About Unknown
Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.