Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeeleza kuwa kiungo mpya wa Yanga,
Pius Buswita anaweza kuanza kuitumikia timu hiyo mara moja baada ya
suala lake kumalizwa kwa malipo.
Yanga
wanatakiwa kurudisha kitita cha Sh milioni 10 ambazo Buswita alichukua
akiwa Mbao FC lakini baadaye akachukua fedha tena na kusaini Yanga na
mwisho amesababisha mtafaruku ambao ulipelekea yeye kusimamishwa kucheza
msimu mzima.
Kwanza
nianze kuwapongeza TFF kufikia hadi kulimaliza suala hilo kwa kuwa
Buswita anaweza kucheza tena na vizuri kwake, familia yake, mashabiki na
hata sisi wadau wa soka kwa kuwa ni kijana ambaye ninaamini akijituma,
baadaye atakuwa msaada kwa taifa letu.