Fashion

Friday, 6 October 2017

URUSI MAMBO SI SHWARI VIWANJA VINAWAKA MOTO

 
Hivi juzi tu raisi wa Urusi Vladmir Putin alisema haridhishwi na uandaaji wa fainali za kombe la dunia, Putin amesema anaona uandaaji wa michuano hiyo nchini hauko sawa na unazua hofu kuhusu michuano hiyo.


Wakati Putin akisema hayo nchi ya Urusi kwa mara ya tatu ndani ya mwaka mmoja imeshuhudi tukio la kuungua moto kwa kiwanja na tena mbaya zaidi uwanja ambao unatarajiwa kutumika kwa ajili ya kombe la dunia.

Nizhny Novogord Stadium ni uwanja ambao umejengwa ukiwa na uwezo wa kuingiza idadi ya mashabiki 45,000, uwanja huu ulishuhudiwa siku ya Alhamisi ukiwaka moto.

Kampuni ya Stroytransangaz ambayo ndiyo watengenezaji wa uwanja huo wamesema wao hawahusiki na mlipuko huo na kusisitiza moto huo hauhusiana kabisa na matengenezo ya uwanja huo.

Hii ni mara ya tatu ndani ya mwaka huu ambapo kiwanja kinaungua nchini Urusi, mwezi wa 6 uwanja wa Volvograd Arena uliungua moto kabla ya mwezi wa nane uwanja mwingine wa Cosmos kushika moto.

Bado miezi 8 tu kwa michuano ya kombe la dunia kuanza kupigwa lakini tayari mashaka yamekuwa makubwa kuhusu michuano  hiyo na suala la viwanja na miundombinu likianza kuzua hofu kubwa.

Unknown

About Unknown

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :