Fashion

Friday 3 November 2017

HARRY KANE ANA NDOTO ZA UBINGWA WA UEFA MSIMU HUU


Kiungo Dele Alli alitikisa nyavu mara mbili dhidi ya mabingwa hao watetezi kabla ya Christian Eriksen kuongeza la tatu 
 
Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur Harry Kane amesema timu yake inaweza kutwaa taji Ligi ya Mabingwa baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Real Madrid Jumatano usiku.

Kiungo Dele Alli alitikisa nyavu mara mbili dhidi ya mabingwa hao watetezi kabla ya Christian Eriksen kuongeza la tatu.
Cristiano Ronaldo aliipa Madrid goli la kufuta machozi lakini Spurs wamefanikiwa kutinga hatua ya mtoano kwa ushindi huo mnono.

"Tunahitaji kuwa na imani," Kane aliwaambia waandishi. "Huenda katika walioshuhudia mchezo ule, hakuna atakayependa kukutana nasi kwenye Ligi ya Mabingwa, timu yetu ni nzuri.

"Tuliingia robo fainali [miaka saba iliyopita] na Madrid walitutoa. Tunajisikia tunaweza kumfunga kila mmoja.
"Ni lazima uifunge timu bora kwenda mbali na hilo ndilo tutakalojaribu kufanya."

Vijana wa Mauricio Pochettino watarudi kwenye Ligi ya Uingereza Jumapili kuikabili Crystal Palace katika uwanja wa Wembley.

Unknown

About Unknown

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :