Fashion

Saturday, 11 November 2017

MWENYE HELA TUNAMPA TUU BANKA ILA TARATIBU MUHIMU



o
Huku habari zikisema Simba na Yanga zinapigana vikumbo kumuwania Mohammed Issa ‘Banka’, klabu ya mchezaji huyo Mtibwa Sugar imesema ruksa kiungo huyo kuondoka ila afuate masharti.

Pamoja na Simba kuhusishwa na mchezaji huyo, kiufundi Yanga ndiyo yenye nafasi kubwa ya kumsajili kiungo huyo kutokana na uhaba wa wachezaji wa aina yake iliyonayo kuliko Simba.

Kocha wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila amesema; timu yoyoye inayomuhitaji kiungo huyo ifuate taratibu za uhamisho ambazo zinafahamika na wao hawana kinyongo.

Mtibwa ni klabu ambayo imekuwa ikitoa wachezaji wengi na wenye vipaji kwenda timu kongwe za Simba na Yanga kwa miaka kadhaa sasa.
“Banka ni mchezaji wetu halali, hivyo kama kuna timu inamuhitaji taratibu zinafahamika cha msingi wafuate hizo taratibu na siyo kupitia njia ambazo si halali. Hatuwezi kuzuia riziki yake.

“Hata mchezaji mwenyewe anajua mkataba wake unasemaje na sisi na kama akipata timu nini anatakiwa kufanya, hatuna tatizo naye na hata timu inayomuhitaji.

“Kwa upande wangu sina mpango wa kusajili mchezaji yeyote kwa sababu kikosi chetu ni kipana, zaidi sasa hivi tunapambana kurekebisha upungufu uliojitokeza katika mechi tisa tulizocheza,” alisema Katwila.

Mtibwa ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 17 katika mechi tisa sawa na Yanga iliyo nafasi ya tatu, lakini imezidiwa mabao ya kufunga na kufungwa. Simba ip

Unknown

About Unknown

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :