Mwalimu wa Taifa Stars, Salum Mayanga amesema wana nafasi ya kufanya vizuri katika mechi ya kirafiki dhidi ya Benini, Jumamosi.
Mayanga amesema watafanya vizuri pamoja na kuwa na pengo la nahodha wake, Mbwana Samatta.
Samatta
ataikosa mechi hiyo kwa kuwa anatakiwa kupata matibabu kwa wiki sita
baada ya kuumia goti akiichezea timu yake ya KRC Genk.
“Tumejiandaa vizuri na tuna nafasi ya kufanya vizuri, tutaimudu Benin,” alisema.
Kumekuwa
na hofu kwa mashabiki wengi ambao wamekuwa wakilijadili suala la Stars
kumkosa Samatta ambaye ndiye tegemeo katika ushambulizi kama kiongozi.