Mchezaji Thomas Ulimwengu
ameondoka katika klabu yake ya AFC ya nchini Sweden na kwenda Ubelgiji
ambako sasa anafanya mazoezi na kikosi cha KRC Genk.
KRC Genk ndiyo klabu anayoichezea Mtanzania mwingine Mbwana Samatta.
Ulimwengu ambaye ni majeruhi wa goti,
ameamua kufanya mazoezi huku akipata matibabu chini ya wataalamu wa
klabu ya Genk ambao sasa wanafanya kazi ya kumtibu Samatta ambaye siku
chache zilizopita amefanyiwa upasuaji.