Fashion

Saturday, 9 April 2016

SPORTS CLUB VILLA YALALA 7 MOROCCO

Klabu ya soka ya FUS Rabat kutoka Morroco ilipata ushindi mkubwa katika mchuano wa mzunguko wa kwanza, hatua ya 16 kuwania taji la Shirikisho barani Afrika kwa kuilemea Sports Club Villa ya Uganda mabao 7 kwa 0.


Mourad Batna ndiye aliyefungua karamu ya mabao kwa klabu yake katika dakika ya 26 ya mchuano huo kwa kupiga mkwaju wa adhabu kutoka katika eneo la hatari.
Kabla ya kipindi cha mapumziko, Mohamed Fouzair aliipa klabu yake bao la pili katika mchuano huo uliopigwa katika uwanja wa Moulay Abdallah mjini Rabat.
Mabao mengine ya FUS Rabat yalitiwa kimyani na Sy Ass Mandaw, Abdessalam Benjelloum, El Mehdi El Bassil, Marwane Saadane na Youssef El Gnaoui
Haya ni matokeo mabaya sana kwa Sports Villa ambayo inaendelea kukabiliana na matatizo ya kifedha na wiki hii ilipata msaada wa Dola 120,000 kutoka kwa rais Yoweri Museveni.
Mchuano wa marudiano utachezwa tarehe 19 au 20 mwezi ujao na Sports Villa Club na inastahili kupata mabao 8 kwa 0 ili kusonga mbele.
Michuano mingine inaendelea siku ya Jumamosi, CS Constantine ya Algeria dhidi ya Misri El-Makasa ya Misri.
Zanaco ya Zambia watakuwa nyumbani kumenyana na Stade Gabesien kutoka Tunisia huku MC Oran ya Algeria wakiwakaribisha Kawkab Marrakech ya Morroco.
Jumapili Aprili 10 2016:-
  • Vita Club Mokanda (Congo) vs Sagrada Esperance (Tunisia)
  • Azam FC (Tanzania) vs Esperance de Tunis(Tnsiia)
  • Al-Ahly Shendi (Sudan) vs Medeama (Ghana)
  • CF Mounana (Gabon) vs ENPPI (Misri)
Ratiba ya Michuano ya Klabu bingwa wikendi hii
Jumamosi Aprili 9 2016

  • Yanga (Tanzania) vs Al-Ahly ( Misri)
  • ASEC Mimomas (Cote Dvoire) vs Al-Ahli Tripoli( Libya)
  • Zamalek (Misri) vs MO Bejaia (Algeria)
  • Wydad Casablanca (Morocco) vs TP mazembe (DRC)
  • Al-Merrikh (Sudan) vs ES Setif (Algeria)
  •  
  • Jumapili Aprili 10 2016
  • AS Vita Club (DRC) vs Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini)
  • Enyimba (Nigeria) vs Etoile du Sahel (Tunisia)
Michuano hii itachezwa nyumbani na ugenini na washindi kufuzu katika hatua ya makundi.

Unknown

About Unknown

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :