Yanga wako Kisiwani Pemba kwa matayarisho yao ya mwisho kabla Jumamosi Aprili 9 kuikabili Al Ahly ya Misri kwenye Mechi ya Raindi ya Pili ya CAF CHAMPIONZ LIGI kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Akiongea Jana kabla ya safari yao ya Pemba, Kocha Mkuu wa Yanga anaetoka Holland, Hans van der Pluijm, amesema Kikosi chake kipo imara na pia kunena: “Naamini tutafanya vizuri ingawa Al Ahly ni Timu nzuri na naamini wao watakuja hapa kujihami zaidi kwani ndio utamaduni wa Timu za huko!”
Kwenye Mechi hii, Pluijm alithibitisha kuwa Mchezaji wao kutoka Rwanda, Haruna Niyonzima, hatacheza kutokana kuwa Kifungoni Mechi 1 kwa kuzoa Kadi za Njano 2 kwenye Mechi zilizopita za michuano hii.
Yanga imefuzu hatua hiyo wa kuitoa APR ya Rwanda kwa Jumla ya Mabao 3-2 kwa Mechi mbili wakati Al Ahly iliibwaga Libolo ya Angola Jumla ya Bao 2-0 baada kutoka Sare 0-0 huko Angola na wao kushinda 2-0 kwao Alexandria.
Mara ya mwisho kwa Yanga na Al Ahly kukutana katika michuano hii ilikuwa Msimu wa 2013/14 ambapo Yanga walishinda 1-0 Mjini Dar es Salaam na Al Ahly kushinda 1-0 huko Misri na Al Ahly kusonga baada ya kushinda kwa Mikwaju ya Penati 5-3.
CAF CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Pili
**Mechi kuchezwa Aprili 8-10 na Marudiano Aprili 19-20
Jumamosi Aprili 9
1600 Young Africans [Tanzania] v Al-Ahly [Egypt]
1830 ASEC Mimosas [Ivory Coast] v Al-Ahli Tripoli [Libya]
2000 Al-Merrikh [Sudan] v ES Sétif [Algeria]
2100 Stade Malien [Mali] v ZESCO United [Zambia]
2100 Zamalek [Egypt] v MO Béjaïa [Algeria]
2130 Wydad Casablanca [Morocco] v TP Mazembe [Congo DR]
Jumapili Aprili 10
1730 AS Vita Club [Congo DR] v Mamelodi Sundowns [South Africa]
1800 Enyimba [Nigeria] v Étoile du Sahel [Tunisia]