Na steve sameo
Msemaji wa Simba Hajji Manara amesema sababu zilizotolewa na wachezaji hao za kucheleweshewa mishahara yao siyo za kweli kwani hadi sasa hakuna mchezaji anayedai mshahara kuanzia Januari mwaka huu.
“Hayo ni maneno yao ambayo hayana ukweli wowote Simba haina deni na mchezaji yeyote kuanzia Januari, wanapaswa kusema ukweli na siyo kudanganya watu,”amesema Manara.
Tayari Kiiza na Mwenzake wamewasili Dar es Salaam, leo asubuhi na wamejiunga na wenzao kambini kujiandaa na mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Coastal Union, utakaochezwa Jumatatu lakini uongozi huo umedai bado utahakikisha unatimiza wajibu wake kwa kuwawajibisha wachezaji hao kwa utovu wa nidhamu walioufanya.