Klabu ya Young Africans itashuka dimbani leo Jumamosi kucheza dhidi ya miamba wa Misri Al Ahly hatua ya 16 bora katika Ligi ya Mabingwa barani Afrika (CAF CL).
Mechi hiyo itachezewa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia saa 10 kamili kwa saa za Afrika Mashariki.
Kocha wa Yanga Hans van der Pluijm, akizungumza awali, alikuwa amesema atahakikisha wanafanya maandalizi mazuri kuweza kuikabili vilivyo timu ya Al Ahly.
Yanga na Azam FC ndio wawakilishi pekee wa Tanzania waliosalia katika michuano.
Azam FC watashuka dimbani Jumapili katika uwanja wa Azam Complex uliopo saa 9 alasiri, kuwakaribisha wenyeji wa Esperance Sportive de Tunis (EST) ya Tunisa.
Kamisaa wa mchezo akiwani Joseph Nkole kutoka nchini Zambia.
Michezo ya marudiano itachezwa Aprili 19-20 mwaka huu.