Beki wa Yanga, Juma Abdul amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa michuano ya Kombe la Shirikisho.
Yanga
ndiyo mabingwa wa Kombe la Shirikisho baada ya kuitwanga Azam FC kwa
mabao 3-1 katika mechi ya fainali kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam, leo.
Wakati
Juma anakuwa mchezaji bora, Kipa wa Azam FC, Aishi Manula ametangwa
kuwa kipa bora na mshambuliaji wa Ndanda FC, Atupele Green ndiye
mpachikaji mabao bora.