Na steve sameo
Msemaji wa TFF Alfred Lucas amesema wamekataa ombi la CECAFA, kwakua wana mambo mengi ya kuyasimamia hivi
sasa moja wapo ikiwa ni ushiriki wa klabu ya Yanga kwenye hatua ya
makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika CAF.
“Hatukuwahi kusema kama tutaandaa michuano ya mwaka huu, na ndiyo
maana tulipokutana na Katibu Mkuu Nicolas Musonye, nikaweka wazi msimamo
wetu mwaka huu tumebanwa sana hivyo tunawaomba CECAFA, kuzungumza na
nchi nyingine ili kuandaa mashindano haya,”amesema Lucas.
Awali mashindano hayo yalipangwa kufanyika Zanzibar lakini baadaye
chama cha soko ZFA, kilikataa kutokana na ukata wa fedha za kuandaa
mashindano hayo na CECAFA kuiomba TFF, ili kuokoa kutofanyika kwa
mashindano hayo mwaka huu.