.Na steve sameo
Ndani ya saa 48 zijazo, klabu ya Manchester United itamtangaza Kocha Jose Mourinho kuwa Kocha Mkuu wa klabu hiyo.
Wakati
Mourinho anatarajiwa kutangazwa, yeye anataka usajili wake wa kwanza
uwe mshambuliaji mkongwe wa Sweden, Zlatan Ibrahimovich ambaye amemaliza
mkataba wake na PSG ya Ufaransa.
Tayari
kuna taarifa zinasema Ibrahimovic yuko tayari kujiunga na Man United
lakini anataka kitita cha pauni million 8 na mshahara wa pauni 200,000
kwa wiki.