Fashion

Saturday 21 May 2016

SERENGETI BOYS KUJITUPA UWANJANI LEO

.


 Na steve sameo
 Serengeti Boys siku ya leo itacheza na Malaysia kwenye mechi yao ya mwisho ya kundi wakisaka ushindi ili kutinga fainali ya 2016 AIFF Youth Cup huko Tilak Maidan Stadium, Vasco, Goa nchini India.


Tanzania mpaka sasa imeshacheza mechi 3 na kuifunga India 3-1 na kutoka Sare na USA 1-1 na kisha South Korea 1-1.

Ili kutinga Fainali Serengeti Boys wanapaswa kuifunga Malaysia ambayo imetoka sare na India na kubondwa na South Korea 3-0.

Ikiwa Serengeti Boys wataifunga Malaysia basi njia yao itakuwa nyeupe ikiwa pia Jumamosi mechi kati ya Marekani na Korea Kusini itaisha kwa timu moja kushinda.

2016 AIFF Youth Cup ni mashindano yaliyoandaliwa na shirikisho la soka la India, All India Football Federation (AIFF), mahsusi kuitayarisha Timu yao ya U-17 kwa ajili ya mashindano ya AFC U-16 na yale ya 2017 FIFA U-17 World Cup.

Mashindano haya yanachezwa kuanzia Mei 15 hadi Mei 25 huko Tilak Maidan Stadium huko Vasco, Goa nchini India,mashindano haya yana hatua mbili za kundi na za mtoano.
Timu 4 za juu za kundi ambalo lina timu 5 zitasonga kuingia mtoano ambapo timu mbili za juu zitacheza fainali.

Unknown

About Unknown

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :