Fashion

Wednesday, 8 June 2016

JAMES RODRIGUEZ AIPELEKA COLOMBIA ROBO FAINALI COPA AMERICA




Colombia imekuwa Nchi ya kwanza kutinga Robo Fainali ya Mashindano ya Copa América Centenario kwa kuibandika Paraguay Bao 2-1 katika Mechi ya Kundi A iliyochezwa huko Rose Bowl, Pasadena, USA asubuhi ya Leo.

Hii ni Mechi ya pili kwa Colombia ambao katika Mechi ya kwanza ya Kundi A waliwatwanga Wenyeji USA 2-0.

Bao za Mechi hii zilifungwa na Carlos Bacca na James Rodriguez katika Dakika za 22 na 30 na Paraguay kufunga lao moja Dakika ya 71 kupitia Victor Ayala.

Kwenye Dakika ya 81 Paraguay walibaki Mtu 10 kufuatia Kadi Nyekundu kwa Oscar Romero baada ya kuzoa Kadi za Njano 2.

Matokeo haya yamefanya Msimamo wa Kundi A baada ya Mechi 2 kwa kila Timu kuwa Colombia wanaongoza kwa kuzoa Pointi 6 na kutinga Robo Fainali wakifuatiwa na USA wenye Pointi 3 huku.

Paraguay na Costa Rica ni za 3 na za 4 wakiwa na Pointi 1 kila mmoja.

COPA AMERICA
RATIBA/MATOKEO:

Saa za Bongo
Jumamosi 4 Juni 2016
USA 0 Colombia 2
Costa Rica 0 Paraguay 0   
Jumapili 5 Juni 2016
Haiti 0 Peru 1        
Brazil 0 Ecuador 0  
Jamaica 0 Venezuela 1     
Jumatatu 6 Juni 2016
Mexico 3 Uruguay 1
Jumanne 7 Juni 2016
Panama 2 Bolivia 1 
Argentina 2 Chile 1 
Jumatano 8 Juni 2016
USA 4 Costa Rica 0 
Colombia 2 Paraguay 1
Alhamisi 9 Juni 2016
0230 Brazil v Haiti  
0400 Ecuador v Peru        
Ijumaa 10 Juni 2016
0230 Uruguay v Venezuela
0500 Mexico v Jamaica     
Jumamosi 11 Juni 2016
0200 Chile v Bolivia

Unknown

About Unknown

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :