Waendesha
mashtaka kutoka mahakama ya kukabiliana na uhalifu nchini Uhispania
wanadai kwamba Neymar na babaake walificha thamani ya uhamisho wa
mchezaji huyo kutoka Santos hadi Barcelona.
Katika mahojiano ya awali Neymar amekana kufanya makosa yoyote.
Hazina moja ya uwekezaji ambayo ilimiliki asilimia 40 ya haki za Neymar indai kwamba haikupata mgao wake kamili. Barcelona inasema kwamba ililipa Yuro milioni 57
kumnunua Neymar mwaka 2013 huku wazazi wake Neymar da Silva Santos na
Nadine Goncalves da Silva Santos akipata wakipokea Yuro milioni 40 na
kilabu yake ya zamani Santos ikipokea Yuro milioni 17.Lakini wachunguzi wanasema kuwa fedha hizo zilifika Yuro milioni 83 na Barcelona ilificha kiasi cha kitita hicho. Klabu hiyo hatahivyo imekana kufanya makosa yoyote.
About Unknown
Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.