Fashion

Tuesday, 7 June 2016

SHERIA ZA TFF ZITAWEZA JUU YA HILI?


.

.Na steven mkeyenge

Timu zinazoshiriki Ligi ya Vodacom Tanzania Bara kuanzia msimu ujao zimetakiwa kuwa na ofisi, Uwanja wa mazoezi, na kuendeleza programu za vijana ikiwemo kuwapa haki ya kusoma.


Msemaji wa TFF Alfred Lucas amesema Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la soka Tanzania TFF ndiyo wametoa sheria hizo wakati ilipokuwa inapitia taarifa mbalimbali za ligi na kukubaliana namna ya kuboresha mashindano mbalimbali ikiwamo Ligi Kuu, Kombe la FA, Ligi Daraja la Kwanza, Ligi Daraja la Pili na Ligi ya Mabingwa wa Mkoa.

"Kamati iliangalia uendeshaji wa Ligi za vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 na Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania TWPL," amesema Lucas.
Aidha, Kamati ya Utendaji imepitisha azimio la kanuni ya leseni ya klabu kuwa ni lazima ianze kutumika msimu mpya wa mashindano wa 2016/17.

Mahitaji ya kanuni hiyo ni pamoja na klabu kuwa na Watendaji wa kuajiriwa kama vile Katibu Mkuu (GS), Mkurugenzi wa Ufundi (TD), Ofisa Usalama (Security Officer) na taarifa ya fedha zilizokaguliwa pamoja na Meneja wa Fedha ambaye atakuwa na uwezo wa kuandaa taarifa za fedha zitakazokaguliwa na wakaguzi wa mahesabu.

Unknown

About Unknown

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :