Kipa
wa Yanga, Deogratius Munish ‘Dida’ ameisaidia timu yake kuanza vizuri
Ligi Kuu Bara kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya African Lyon.
Lakini wakati akiwa uwanjani, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, baba yake mzazi aliyekuwa amelazwa amepoteza maisha.
Imeelezwa,
kwamba pamoja na Yanga kupata taarifa hizo za msiba, waliona haikuwa
sawa kumueleza wakati wa mapumziko, hadi baada ya mechi, alielezwa jambo
hilo.