Mwanariadha wa Ethiopia Almaz Ayana
ameishindia Afrika dhahabu ya kwanza Michezo ya Olimpiki mjini Rio na
kuvunja rekodi ya dunia mbio za mita 10000 wanawake.
Rekodi ya awali iliwa 29:31.78 na iliwekwa na Mchina Wang Junxia mwaka 1993. Mkenya Vivian Cheruiyot ameshinda fedha naye raia mwingine wa Ethiopia Tirunesh Dibaba akachukua shaba.