Katibu mkuu wa Simba Patrick Kahemela amesema wanataka kuanza safari hiyo mapema kwa ajili ya kuwapa mapumziko wachezaji wao na ili waweze kushinda mchezo huo unaotarajiwa kuwa mgumu kutokana na ushindani uliopo.
“Maandalizi yetu yanaendelea vizuri na kwa kasi tuliyoanza nayo tumepanga kwenda mapema Mbeya lakini tunapitia Iringa kwa ajili ya mchezo mmoja wa kirafiki pia kuwasalimia mashabiki wetu ambao hawajaiona timu yao kwa muda mrefu,” amesema Kahemela.
Kocha Omog ametoa tahadhari kwa wachezaji wake kuwa makini katika michezo ya mikoani kwani wanaweza kujikuta wanavuruga rekodi yao ya kutofungwa kutokana na ushindani na ubovu wa viwanja vya mikoani.