Makamu
Mwenyekiti wa Azam, Idrissa Nassor ‘Father’, amesema vyovyote
itakavyokuwa lazima wakiimarishe zaidi kikosi chao kwenye usajili wa
dirisha dogo utakaoanza Novemba 15, mwaka huu.
Azam
ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 22 ambapo kwenye mechi 13, imeshinda
sita tu na kupoteza tatu ikiwa na sare nne, mwendo ambao Father
anaamini siyo wa kawaida kwa timu yao.
Tayari
Kocha Zeben Hernandez amewataarifu viongozi wa Azam kuhakikisha
anaongezewa nguvu kwenye ushambuliaji ambapo Father amesema kuna sura
mpya tatu za washambuliaji watakaosajiliwa.
“Washambuliaji
wawili watatoka nje ya nchi na mmoja wa hapahapa nchini, tunataka
kuhakikisha wanampa sapoti kubwa John Bocco katika kusaka ushindi,”
alisema Father.
Father
amesema kuwa katika kutekeleza hilo, watamleta fowadi wao Mghana Enock
Ageyi ambaye anacheza Medeama kwa mkopo huku mikakati ya kusaka straika
mwingine wa kimataifa ikirarajiwa kuanza muda wowote.
“Kweli
mikakati ya kuboresha kikosi ipo na kwa kuanza kocha ameomba kuongezewa
nguvu kwenye ushambuliaji. Mmoja tunataka awe mzawa na mwingine wa
kimataifa ambaye ataungana na Ageyi ambaye tulimuacha kwa mkopo Medeama,
naye anakuja ili kujaribu kumuongezea nguvu Bocco,” alisema Father.
“Kwa
ujio wa Ageyi tutakuwa na wachezaji wa kigeni zaidi ya kanuni, hivyo
lazima tumuache au tuwaache wengine ili kupisha hao wapya.”
Waivory
Coast, beki kisiki, Pascal Wawa na Frasciso Zukumbariwa huenda safari
ikawakuta kutokana na mchango wao mdogo katika timu kwani Wawa hajacheza
mechi yoyote msimu huu ikidaiwa haelewani na Zeben.