Fashion

Tuesday 22 November 2016

ZLATAN KUJENGEWA SANAMU SWEDEN



.
Chama cha Soka cha Sweden (SvFF) limetangaza kutengenezwa kwa sanamu maalum la mshambuliaji nyota wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic.

Zlatan ni mchezaji wa timu ya taifa ya Sweden na nahodha, lakini ni Mswidi aliyeshinda tuzo ya mwanamichezo bora wa Sweden kwa miaka 10 mfululizo.

Sanamu lake litawekwa nje ya Friends Arena katika jiji la Stockholm.

Hali hiyo ni kuonyesha kuthamini mchango wake akiwa na timu ya taiga ya Sweden lakini kuwasaidia wanamichezo chipukizi kuhakikisha wakiwa na hamu ya kupata mafanikio.

Zlatan ambaye sasa ana umri wa miaka 36, akiwa na timu ya taifa ya Sweden amecheza mechi 114 na kufunga mabao 62. Alitangaza kustaafu baada ya michuano ya Euro iliyofanyika nchini Ufaransa, hivi karibuni.

Unknown

About Unknown

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :