Mshambuliaji wa Man City, Kun Aguero atakosa mechi nne za Ligi Kuu England baada ya kufanya rafu ya kijinga dhidi ya beki David Luiz wa Chelsea.
Chelsea
iliitwanga Man City kwa mabao 3-1 na Aguero akamrukia Luiz katika
dakika ya 90. Pamoja na kadi nyekundu, FA imeamua akose mechi hizo nne.
Wakati
Aguero anakosa mechi nne, kiungo Fernandinho naye atakosa mechi tatu
akitumikia adhabu ya kumkaba kooni na kumsukuma hadi chini kiungo Cesc
Fabregas.
Luiz amekataa katakata kulizungumzia suala kwamba, huenda amekuwa na ugomvi na Aguero ambaye katika mechi hiyo, yeye alianza kumngonga.
04
Dec
2016
Luiz amekataa katakata kulizungumzia suala kwamba, huenda amekuwa na ugomvi na Aguero ambaye katika mechi hiyo, yeye alianza kumngonga.