Mheshimiwa, Mwigulu Nchemba ambaye ni shabiki wa Yanga wa
‘kutupwa’, amekutana na kiungo mpya wa Yanga, Justice Zulu.
Zulu raia wa Zambia, yuko nchini tayari kumalizana na Yanga.
Mwigulu ambaye ni straika tegemeo wa Yanga katika timu ya Wabunge ameonekana akiwa picha na Zulu, nje ya hoteli aliyofikia.
Zulu
anatarajia kumalizana na Yanga, leo au kesho na mara moja ataanza kazi
katika harakati za kocha mpya, George Lwandamina kuandaa kikosi chake.