CHAMA CHA SOKA MKOA WA MBEYA
KIMEZAMILIA KUFANYA MDAHARO NA WADAU WA SOKA MKOANI HAPA.
Akizungumza na waandashi wa
habari mwenyekiti wa chama cha soka mkoani
Mbeya (MREFA) Eliasi mwanjala amesema dhumuni kubwa ni kutathimini
mwenendo wa timu za mkoa ambazo ni Prison na Mbeya city zinazoshiriki ligi
kuu Tanzania bara maarufu Vpl kuwa
zinabaki katika ligi kuu .
Pia Mwanjala hakubaki nyuma
na kuziangazia timu zinazoshiriki ligi daraja la kwanza na la pili ambapo Mbeya
inawakilishwa na timu ya Mbeya kwanza inayoshiriki daraja la kwanza na Mbarali
united inayoshiriki daraja la pili kuwa zinafanya vizuri na kupanda madaraja
ili kuongeza timu katika ligi kuu zinazotokea mbeya.
Mdaharo huo utafanyika tarehe
9/1/2017 katika ukumbi wa Mkapa hall kuanzia saa nne mpaka saa 9 mchana utakuwa
mahususi kwa ajili ya kuongeza hamasa ya
soka mkoani na ushirikiano kati ya
viongozi wa mpira kutoka mkoani hapa na wadau /mashabiki kuleta ufanisi katika
soka bila kusahau wadau wa soka kuchangia mawazo yao kuleta tija katika soka la
mkoa .
.Mgeni rasmi katika mdaharo
huo atakuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya mheshimiwa Amosi Makala ambaye atakuwepo na
kusikiliza kero mbali mbali za kandanda mkoani hapa .
Hata hivyo Mwanjala ameomba wadau kujitokeza kwa wingi
katika mdaharo huo ili kuzungumzia swala la mpira wa mkoa pamoja na kero
walizonazo katika soka mkoani hapa