Sunday, 8 January 2017
DC CHUNYA AONGOZA VIONGOZI KWENYE HARAMBEE MAKONGOLOSI
Viongozi wa Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya wamelazimika kufanya harambee ili kuinusuru Zahanati ya Kijiji cha Makongolosi isifungwe kutokana na ukosefu wa choo kwa muda mrefu sasa.
Harambee hiyo iliongozwa na Diwani wa Kata ya Bwawani Mheshimiwa Sailon Mbalawata na kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa, Mbunge wa Chunya Victor Mwambalaswa,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Sophia Kumbuli na Diwani wa Mkola na Matundasi.
Gharama za ujenzi wa choo hicho ni zaidi ya shilingi milioni nane na katika harambee hiyo zaidi ya shilingi milioni saba zilipatikana.
Mbunge Mwambalaswa alichangia zaidi ya shilingi milioni mbili, Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa alichangia zaidi ya shilingi milioni moja na Mkurugenzi Sophia Kumbuli alichangia milioni moja.
Pia baadhi ya vikundi na jumuia za Chama Cha Mapinduzi zilichangia pesa na mifuko ya saruji. Mkuu wa Wilaya amewataka wananchi kuchangia maendeleo kwani Zahanati hiyo itawaondolea adha wananchi wa Bwawani na Makongolosi.
About Unknown
Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.