Striker wa Yanga, Simon Msuva amesema wamekikubali kipigo kutoka Azam FC lakini bado wana nafasi ya kujirekebisha.
Yanga
imepokea kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Azam FC katika mechi ya mwisho
ya Kundi B katika michuano ya Mapinduzi. Mechi hiyo imechezwa jana
kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Msuva amesema mashabiki wasikate tamaa, waendelee kuwaunga mkono nao kupitia benchi la ufundi na wao wenyewe watajirekebisha.
"Mpira
una matokeo matatu, kushinda, sare au kufungwa. Kufungwa imetutokea
sisi, lakini hatuna ujanja. Nawaomba mashabiki wasikate tamaa na badala
yake waendelee kutuunga mkono.
"Benchi la ufundi wameona makosa yetu, sisi wachezaji tumeona na tutayafanyia kazi na kuendelea kufanya vizuri.
"Unajua
kikubwa ambacho ni kizuri tumevuka kwenda nusu fainali hivyo tuna
nafasi ya kujirekebisha kwenye nusu fainali na ikiwezekana fainali,"
alisema.