Wednesday, 11 January 2017
DC CHUNYA AHAMASISHA UJENZI WA VYOO BORA KUEPUKANA NA MAGONJWA YA MLIPUKO
Katika kuhakikisha wananchi wa Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya hawakumbwi na magonjwa ya mlipuko yanayotokana na ukosefu wa vyoo mkuu wa Wilaya hiyo Rehema Madusa ameanza ziara ya kushitukiza katika Kata mbalimbali ili kufanya ukaguzi wa vyoo katika kaya na Taasisi za serikali na dini zina vyoo vya kisasa .
Madusa amesema kuwa lengo la ziara yake ni kuhimiza kila mwananchi anakuwa na choo ili kuepukana na magonjwa ya kipindupindu au yanayotokana na mkojo.
Hivi karibuni mkuu wa Wilaya amefanya ziara katika Kata ya Chokaa na Sangambi katika vijiji vya Shoga,Igundu, Godima na kujionea kaya nyingi na Taasisi ambazo hazina vyoo hivyo kuwa katika hatari ya kukumbwa na magonjwa.
Aidha katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya amehimiza wananchi kukamilisha ujenzi wa madarasa mapya, nyumba za walimu na Zahanati ili kuondoa adha kwa wananchi ambapo ametoa miezi miwili kukamilika kwa majengo katika vijiji alivyotembelea,
Hata hivyo ametoa mwezi mmoja kwa kila kaya Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kuwa na choo na atakayekiuka anakabiliwa na faini ya shilingi laki mbili au kifungo Gereza ni.
Madusa amesema hatakuwa tayari kuona mwananchi wa Wilaya ya Chunya anakufa kwa magonjwa yanayoweza kuepukika.
About Unknown
Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.