. Baraza
la madiwini Halmashauri ya wilaya ya Mbeya vujijini mkoani hapa limepitisha Zaidi
sh 65 bilioni kwa mwaka wa fedha
2017/18.
Akiwasilisha bajeti hiyo jana afisa mipango wa halmashauri
hiyo Anyambilile Mwandiga alisema bajeti hiyo inalenga kuboresha huduma kwa wananchi
ikiwemo huduma za afya,uhaba wa vyumba madarasa,maji na maabara kwa shule za
sekondari.
Mwandiga
aliongeza kuwa kati ya fedha hizo,ruzuku kutoka serikali kuu ni kwa ajiri ya
mishahara ya watumishi, matumizi mengineyo na maendeleo ni sh 62 bilioni Huku mapato
ya ndani ikiwa ni sh 2 bilioni.
Kaimu
mkurugenzi wa halmashauri hiyo Abihudi Fungamtama alisema bajeti hiyo imelenga
kutekeleza miradi mbalimbali ambayo imetengewa fedha.
“hii bajeti
itaenda kupunguza baadhi ya changamoto ambazo wananchi wanakumbana nazo hasa
uhaba wa madawa,barabara,maji na elimu”alisema Fungamtama.
Hata hivyo
mwenyekiti wa halmashauri ya Mbeya Mwalingo Kisemba alisema katika mwaka wa
fedha unao isha juni 30 mwaka huu kumekuwa na changamoto ya ukusanyaji wa
mapato kutokana na zao la pareto kukosa soko na kuchelewa kwa mvua kunyesha
kwani halmashauri hiyo inategemea mapato yake kutoka kwa wakulima.
Aidha
Kisemba aliongeza kuwa mwaka wa fedha ujao wamejipanga kuimarisha uzalishaji wa
zao la kahawa na pareto ili kuongeza asilimia kadhaa katika mapato yake.