Na hiyo inatokana na timu ya taifa, kutokuwa na mchezo wowote wa kirafiki wa kimataifa tangu Desemba, licha ya kutofuzu Fainali za Kombe la Mataifa (AFCON) nchini.
Tanzania kuangukia nafasi ya 158 ikiwa na pointi 152 katika orodha ya Februari, 2017 inamaanisha imeshuka kwa nafasi mbili zaidi kutoka ya 156.
Pamoja na kuporomoka kwa nafasi mbili hadi ya 73, lakini Uganda wameendelea kuongoza kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati.
Na Uganda imeporomoka Januari kutokana na kutoshinda mechi katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka huu Gabon. Kenya ni ya pili kwa ukanda wa CECAFA ikiwa nafasi ya 87.
Mabingwa wapya wa Afrika, Cameroon wamepanda kwa nafasi 29 hadi ya 33, huku washindi wa pili Misri wamerudi juu hadi nafasi ya 23 baada ya kuporomoka miaka miwili iliyopita.
Tanzania inaingia katika zama mpya sasa chini ya kocha Salum Mayanga, anayekuwa kaimu kocha Mkuu wa Taifa Stars akirithi mikoba ya Charles Boniface Mkwasa aliyeondolewa mapema mwezi huu.