Fashion

Saturday 11 February 2017

WAWAKILISHI WA KLABU BINGWA TANZANIA YANGA SC TAYARI KUWAVAA WA COMORO



Kikosi cha Yanga SC kimeondoka Alfajiri ya leo asubui kuelekea nchini Comoro kwenye mji wa Moroni  tayari kwa mchezo wake wa kwanza ya Ligi ya mabingwa dhidi ya Ngaya.

Msafara utakuwa na wachezaji ishirini(20) benchi la ufundi nane( 8 )pamoja na viongozi wawili(2).

Wachezaji wanaoondoka kesho ni.

Deogratius Munish, Ally Mustafa,Deud Kaseke,Haruna Niyonzima,Thaban Kamusoko, Amissi Tambwe, Mwinyi Haji, Saimon Msuva, Geoffrey Mwashuiya,Saidi Makapu, Hassan Ramadhani, Juma Mahadhi, Yusuph Mhilu, Obrey Chirwa, Nadir Haroub, Justine Zulu, Kelvin Yondani, Juma Abdul, Oscar Joshua na Emmanuel Martin.

Benchi la ufundi wanaoondoka ni:

George Lwandamina,Noel Mwandila,Edward Samwel Bavu,Juma Pondamali,Juma Zakaria Omary,Hafidhi Saleh Suleiman,Mohamed Omary Mwaliga na Jacob Sospeter Onyango.

Viongozi wanaosafiri.

Mussa Mohamed  Kisoki (TFF) na Paul Malume (Yanga Sc)

Baada ya kikosi kuwasili kinatarajiwa kufanya mazoezi yake kesho jioni kwenye uwanja utakaochezewa mchezo siku ya jumapili.

Imetolewa na Idara ya Habari na mawasiliano.
Young Africans Sports Club

Unknown

About Unknown

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :